Tetesi za Soka Ulaya
Mshambulizi wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 24, anataka kitita cha pauni milioni 206 ili kujiunga na klabu yoyote msimu huu wa joto. (Mail)
Beki wa RB Leipzig na Croatia Josko Gvardiol, 21, anakaribia kujiunga Manchester City kwa mkataba wa pauni milioni 86. (Telegraph - usajili unahitajika)
Mkufunzi wa Fulham Marco Silva, 45, amekataa ofa ya kandarasi ya pauni milioni 17 kutoka kwa Saudi Pro League. (iNews - usajili unahitajika)
Aymeric Laporte anavutiwa na vilabu vya Arsenal na Juventus, huku mustakabali wa beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 katika klabu y Manchester City ukikumbwa na hali ya sintofahamu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
AC Milan wametoa ofa ya euro mioni 14 kumnunua winga wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24. (The Athletic - usajili unahitajika)
Manchester City wana nia ya kumuuza beki wa Uingereza Kyle Walker, 33, ambaye amekuwa akiwindwa na Bayern Munich, na wanatarajiwa kumpa mkataba mpya. (Fabrizio Romano)
Brentford wamekubali ada ya pauni milioni 23 kutoka Wolves ya kumsajili beki wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, 22. (Sky Sports)
Mabingwa wa Serie A Napoli wanahofia dau la euro 35m likikataliwa na Wolves kwa ajili ya beki wao mwingine Mwingereza Max Kilman mwenye umri wa miaka 26. (The Athletics - Usajili unahitajika)
Mchezaji wa zamani wa Fulham anayeichezea kwa mkopo Manor Solomon, 23, anatazamiwa kujiunga na Tottenham, huku wachezaji hao wa London wakikubali mkataba wa miaka mitano na mchezaji huyo wa kimataifa wa Israel baada ya kandarasi yake na Shakhtar Donetsk ya Ukraine kusitishwa. (The Athletics - Usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United na Nottingham Forest Jesse Lingard, 30, anafanya mazoezi na klabu ya MLS Inter Miami, licha ya Wayne Rooney kupuuzilia mbali tetesi kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza atajiunga na DC United. (Mirror)
Mlinda mlango wa zamani wa Juventus, Paris St-Germain na Italia Gianluigi Buffon, 45, amepewa ofa ya pauni milioni 25 kwa mwaka ili kuhamia Saudi Pro League. (Mail)
Benfica wanakaribia kumsajili winga wa Juventus mwenye umri wa miaka 35 Angel Di Maria, ambaye alishinda Kombe la Dunia la 2022 akiwa na Argentina. (Fabrizio Romano)
Sergio Ramos, 37, ametambuliwa kama shabaha ya pili ya Inter Miami, huku klabu hiyo ya MLS ikimtaka beki huyo wa zamani wa Paris St-Germain baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania kuwa mchezaji huru hivi majuzi. (Mirror)
Mlinzi wa zamani wa Arsenal Konstantinos Mavropanos atagharimu Nottingham Forest 'kati ya £13m na £17m' iwapo atajiunga nao kutoka Stuttgart, huku Eintracht Frankfurt na Napoli pia zikimwania mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki mwenye umri wa miaka 25. (Mail)
Luton Town wanajadiliana na Birmingham City kuhusu usajili wa winga wa Uholanzi Tahith Chong, 23, kutoka klabu hiyo ya Championship. (Mail)
Habari kutoka BBC
https://www.bbc.com/swahili/articles/c809zrd36y9o
No comments