Trending Now

NYOTA WAKO



            Jina lake Halisi ni Gangasani Rami Reddy ambae

Amezaliwa tarehe 1 Januari 1959. Alikuwa mwigizaji ambae alifanya kazi kupitia filamu zä Kihindi Telugu, Tamil, na Kimalayalam. 

              Pia alifanya kazi kama mkurugenzi na mtayarishaji. Anajulikana kwa kuigiza majukumu yake mbaya (adui), na pia majukumu komedi. Alikuwa mhalifu aliyejulikana sana na alikuwa na mindo usio na kifani wa lahaja ya kawaida ya Telangana (swaga).

            Kabla ya kuingia katika filamu, Reddy alifanya kazi na Mf Daily kama mwandishi wa habari. Alijipatia umaarufu kwa jukumu lake kama 'Spot Nana' katika filamu ilivovuma sana ya Ankusam ambayo ilimpatia tuzo ya Adui bora Mwaka 1989 kupitia tuzo zà Nandi Awards na filamu zingine zikiwemo Osey Ramulamma, Ammoru, Gaayam, Anaganaga Oka Roju na Peddarikam. 

             Aliigiza katika filamu zaidi ya 250 kama mhalifu na mwigizaji mhusika katika lugha za Kitelugu, Kitamil, Kikannada, Kihindi, Kimalayalam na Bhojpuri.

          Rami Reddy alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya ini na figo. Na mnamo tarehe 14 Aprili 2011 alifariki dunia katika hospitali ya kibinafsi aliyokuwa akipatiwa matibabu huko Secunderabad na alifariki

Akiwa na umri wa miaka 52 tu alipokufa.


Je ungependa kujua zaidi juu ya NYOTA WAKO?.

No comments